top of page
depositphotos_5030160_m.jpg

Taarifa ya Mradi Mbadala

Haki ya Elimu kwa Ajili ya Mabadiliko ya Jamii:
Mfumo wa Utendaji

Sisi, wahusika tulioweka sahihi zetu, tunaamini kwamba mipango ya sasa ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, na kielimu inazaaa mahusiano ya madaraka ambayo yanasababisha ukosefu mkubwa wa usawa  na ambao hatimaye utatishia maisha katika sayari hii.  Msimamo wetu ni mafunzo mbadala kwa ajili ya haki, na mfumo wa elimu unaokwenda na wakati ambao utasaidia mabadiliko ya kijamii tunayohitaji ili kuunda ulimwengu tajiri, wenye usawa zaidi, na endelevu.

Majanga yaliyopo ulimwenguni na yale yanayohusiana nayo yanasukuma ubinadamu na sayari hai kuelekea mwangukowa kisiasa, kijamii, kiuchumi, na kiikolojia. Majanga haya - ambayo kwa sasa yanaonekana katika janga la coronavirus duniani kote, kutokuwepo kwa usawa wa kimuunitikadi, ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi, muundo dume uliojikimu, kuongezeka kwa machafuko ya hali ya hewa na mazingira, na tishio la mara kwa mara la vita - yanaendeshwa ulimwenguni na ubepari na harakati za kijeshi. Lazima tuchukue wakati huu wa kipekee wa kihistoria ili kufikiria upya na kubadilisha elimu ya umma kwa kiasi kikubwa kama hatua ya kuingia kwenye mabadiliko ya kina ambayo yatajenga mshikamano wa kibinadamu na ushirikiano na kuleta mwisho wa ubaguzi wa rangi, muundo dume, na ubepari. Tunakataa wazo kwamba kipaumbele cha elimu ni kujenga 'mtaji wa nguvumali'; tunasisitizai kwamba vipaumbele vya elimu vinapaswa kujumuisha mifumo ya ikolojia endelefu r na haki zaidi za kijamii kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Hii inahitaji kuundwa kwa mifumo ya haki ya elimu ambayo tunaweza tu kufikia kama sehemu ya mapambano mapana kwa ajili ya mabadiliko ya kijamii katika nyanja nyingine zote, hasa uchumi na katika siasa.

 

Mapambano ya kimaendeleo ni muhimu kuunda mikataba mipya ya kijamii ambayo hutumikia maslahi ya pamoja ya wengi badala ya maslahi binafsi ya wachache. Historia ya binadamu inaonyesha mfululizo wa mabadiliko magumu na yanayohusiana ya kijamii yaliyoundwa na mahusiano ya madaraka: kuanzia nyakati za ujima hadi viwanda, kupitia ushindi wa kikoloni, udikteta wa kimabavu, baada ya ukoloni, utandawazi wa ubepari mamboleo, mapinduzi ya kidijitali na ushirikiano kati ya upelelezi wa kibepari i na hali ya usalama wa taifa tunaona leo. Kila tabaka  jipya linalotawala linazalisha itikadi inayoendeleza utawala wake, na kuahalalisha kutokuwepo kwa usawa, linajenga, na kukuza ukataji wa tamaa kwamba mabadiliko yanawezekana Mamlaka  haya ya kiitikadi karibu daima huhusisha uzingatiaji, na kuunda mifumo ya elimu inayoimarisha dhana za kitabaka na mawazo amabayo ni magumu kuyabadili - binadamu/zisizo za kibinadamu, kiume/kike, akili/mwili, kidunia/kiroho, bora/duni, mijini/vijijini, sisi/wao - ambayo humpa mshindi  haki ya kutumia ulimwengu wa asili na viumbe vyote vinvyoishi. Udikteta mamboleo, uzawa, mfumo dume, na umaarufu wa ulowezi wa kikoloni unaojitokeza duniani kote baada ya ujio wa utandawazi na ongezeko la uhamiaji kutokana na migogoro na mabadiliko ya tabia nchi yanaimarisha upinzani huu wa pande mbili na kuchochea ukosefu wa usalama wa kijamii ili kukaza mshikilio wao. 

 

Leo, mifumo ya elimu duniani kote imeundwa katika mawazo ya ubepari mamboleo na mawazo ya ufanisi, kiwango cha kurudisha mtaji, uchaguzi, ushindani, na ukuaji wa uchumi. Itikadi hii inayapa mashirika tajiri ya kimataifa na mabilionea  uwezo usio na vizuizi wa kuunda mwelekeo wa uchumi wa dunia na mifumo ya kisiasa ya kitaifa, na kuendelezauchimbaji madini na, shughuli za kiuchumi zinachafua hewa na kusababisha matumizi yasiyozuilika na uharibifu mkubwa wa mazingira. Ikiwa imepangwa kwa namnaa hii, mifumo ya elimu hutumika kuimarisha na kuhalalisha hali ya kutokuwepo usawa wa kijamii, ubaguzi, na matabaka ndani ya mataifa yote. Hata hivyo, kama zinavyoonyesha tawala zilizopo, elimu pia ni uwanja muhimu wa mashindano. Mataifa ya kimabavu, yakijua vizuri sana kwamba elimu inaweza kuwa nguvu ya mabadiliko, yanachukua hatua za haraka kuitumia kama chombo cha kuhakikisha watu wanadhibitiwa na kutii.

 

Matokeo yake, kwa watoto wengi na vijana, hakuna matumain ulimwengu. Ubora wa elimu wanayoipata unazidi kutenganiswana hadhi yao katika jamii na kiuchumi na eneo la kijiografia wanapokaaa familia zao. Elimu inazidi kupangwa katika masoko ya ushindani ambayo yanaunda na kukita  ukabila, tabaka, na ukosefu wa usawa wa kijinsia ambapo wenye shule binafsi na wakandarasi, pamoja na walimu na wanafunzi wanashindana kupitia, na wanapimwa kwa kutumia ufanisi wa gharama na viwango vya mitihani: Elimu iliyofanywa kama bidhaa inayotolewa kupitia bajeti za ummaamabazo hazitoshelezi, huzingatia ubora wa matokeo, uundaji wa mtaji wa nguvumali, na kiwango cha urudishaji wa mtaji kiuchumi, na thamani ya pesa. Aina hii inaimarisha matabakaya binadamu, ubaguzi wa rangi, wazungu kujiona ndio bora na watawala, unyanyapaaji wa walio tofautii, uhalalishaji wa ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kisiasa, ubinafsi wa kupitiliza, uchumi usiokua , mapokezi bila ukosoaji waa matangazo yenye makidai, na ufuataji wa sheria za kimabavu. Tokeo lake moja ni utata wa kupindukia kwamba jamii zilizoelimika sana katika historia ya binadamu kwa pamoja ndizo zinazosababisha kuanguka kwa mifumo ya sayari hai, ambacho ni kama kitendo cha kujiua kwa pamoja na uharibifu wa mazingira.

 

Kwa miaka thelathini iliyopita, mapekendezoi endelevu ya asasi za kiraia na vyama vya elimu yamesukuma ulimwengu kukumbatia haki ya elimu na dhamira ya Elimu Kwa Wote: Kwenda shule kwa lazima kumepanua kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa – kwa kuwashirikisha watoto karibu bilioni mbili kila siku. Familia nyingi sasa zinaamini kwamba kumaliza miaka 8 hadi 12 ya shule ni muhimu kwa mustakabali wa watoto wao na serikali nyingi zinaamini kwamba kutoa elimu bure kwa umma kwa watoto wote na vijana ni sera nzuri ya umma. Lakini hatupo karibu na kufanikisha hili. Kwa sehemu, udhalimu mkubwa wa kimuktadha ulilaosababishwa na miongo minne iliyopita uliozingatia masoko kama msingi umesababisha kudumishwa kwa matumizi madogo katika sekta ya kijamii na kubeza shughuli zote za serikali kama "zisizofaa" na “matumizi mabaya." Matokeo yake, uwekezaji kwenye elimu umekuwa hautoshi, na uwekezajii zaidi unahitajika na inawezekana, kutoka kwa serikali za kitaifa na pia mashirika ya kimataifa na ya kimataifa. 

 

Sio kwamba hakuna pesa; serikali daima hupata fedha za kutumia kwa ajili ya jeshi, polisi, usalama naupelelezi, na ustawi wa makampuni. Ili kukabiliana na itikadi hii, ni lazima tufichue uhaba kama hadithi na ubanaji matumizi  kama chaguo la sera ya makusudi ya kuendesha ajenda ya ubinafsishaji  unaotokana na upebari mamboleo.

 

Wakati malengo ya matumizi kwa ajili ya elimu yanaakisi makubaliano ya kimataifa, serikali nyingi hazifikii hata lengo la kutumia asilimia 20 ya bajeti zao na asilimia 6 ya Pato lao la Taifa kwa ajili  ya elimu. Jumuiya ya kimataifa imeahidi kwa miongo kadhaa kutumia asilimia 0.7 ya Pato lao la Taifa kama Msaada Rasmi wa Maendeleo, lakini bado wanatenga kisehemu kidogotu cha hii. Na malengo haya yote yanadhoofisha sana wahitaji. 

 

Tunahitaji kushinda hoja hizi katika nyanja za umma. Tatizo liliko ni zaidi ya uwekezaji. Taasisi za fedha za kimataifa -- kama vile IMF na Benki ya Dunia -- ni taasisi za ukoloni mambaleo zinazoendeleza sera za upebari mambaleo, kile kinachojulikana kama sera za Makubaliano ya Washington duniani kote. IMF na Benki ya Dunia zimekuwa na jukumu kubwa la ushawishi katika sera ya elimu (na sera nyingine za kijamii). Badala ya kusaidia elimu, IMF kwa kweli inazuia nchi kutumia pesa kwa ajili ya kuajiri walimu na watumishi wengine wa sekta ya umma. Benki ya Dunia inajifanya kuwa chanzo cha utafiti wa ushauri wa malengo mazuri, lakini kwa miongo minne iliyopita imeweka mapendekezo yake katika itikadi yake ya ubepari mamboleo. Ni wakati muafaka kwa mkutano mpya wa Bretton Woods kwa ajili ya kufikiria marekebisho makubwa ya IMF na Benki ya Dunia. 

 

Tunatoa wito wa mabadiliko makubwa. Serikali zote lazima zifanye elimu ya umma bure tangu utotoni hadi elimu ya juu ambayo itawezesha umuhimu, ushirikishaji, wa kidemokrasia na kutathimini namna tunavyo fikiria  kutenda pamoja duniani kote. Kutoa elimu kama haki ya binadamu inahitaji uwekezaji kamilifu katika mifumo ya umma, uwekezaji endelevu kupitia mifumo ya kitaifa na kimataifa, marekebisho ya mfumo wa kodi, pamoja na msaada usio na masharti kutoka jumuiya ya kimataifa. Mtaala unapaswa kukataa kikamilifu ukimya na ushiriki  wa watumiaji wa huduma ambao hulisha ongezeko la joto duniani na janga la hali ya hewa. Ikiwa na mizizi yake katika jamii, elimu lazima iwe muhimu kiutamaduni na kukuza maadili ya kibinadamu ya kupinga ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia, na kujenga, mshikamano wa kijamii, huruma, fikira, ubunifu, utimilifu wa kibinafsi, amani, uongozi unaojali mazingira, na kuimarisha demokrasia. Waalimu wanahitaji uhuru wa kitaaluma, mazingira bora ya kazi, na, kupitia vyama vya wafanyakazi na mashirika mengine, sauti kubwa katika utengenezaji wa sera. Kadhalika, wanafunzi na vyama vyao vya uwakilishi lazima pia wawe na sauti katika maamuzi ya kisiasa na kiakademia, wakiwa kwamba haki yao ya kushiriki imetambuliwa kikamilifu. 

 

Dunia inahitaji mtazamo wa kina wa elimu ambayo itasaidia kubadilisha na kuunda jamii zenye mabadiliko. Hii itahitaji mkataba mpya wa kijamii ambao unathamini matumizi kwa ajili jamii juu ya matumizi ya kijeshi na usalama na kwenda zaidi ya maslahi finyu ya sekta ya biashara, makampuni ya technologia za elimu, minyororo ya shule binafsi, na wadau wengine wa biashara ya elimu. Tunatoa wito wa kugeuza harakati za kuelekea ubinafsishaji wa elimu na huduma zingine za kijamii na kuweka mantiki ya biashara nje ya elimu na upangaji wa sera za kijamii.

 

Badala yake tunapata nguvu kutokana n mapambano na kujifunza kutoka kwa jumuia za wanafunzi na walimu, harakati za vyama vya wafanyakazi kwa ujumla, jumuia za za kidemokrasia za kijamii - ikiwa ni pamoja na vyama vya walio wachache, wahamiaji na wakimbizi -  na pia vyombo huru vya habari, vyama, na wataalamu ambao ni washirika wa ahadi yetu ya kuendeleza haki katika jamii halisi  tunamoishi na dosari zake. Makundi haya tayari yameandaa njia mbadala za haki za kielimu, ikiwa ni pamoja na shule na programu zisizo rasmi za elimu zinazosaidia ujamaa wa karne ya 21, uhuru wa wazawa na watu weusi, kuondolewa kwa ukoloni, harakati za umuhimu wa maisha ya watu weusi,   na mafunzo muhimu.

 

Haki katika elimu inategemea uendelezajiwa malengo yanayohusiana na haki katika maeneo manne:

1. Haki ya kijamii - Kujenga elimu kwa ajili ya usawa, mageuzi, na maisha yanayobadilika.

Mifumo ya elimu inahitaji kurudi tena katika kushughulikia ukosefu wa usawa na haki katika jamii zao, kukuza haki za binadamu wa  wa rangi zote, jinsia, na ulemavu, na aina shirikishi ambazoo zitafundisha jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja na kuendesha mabadiliko ya elimu na jamii. 

2. Haki ya hali ya hewa - Kujifunza jinsi tunaweza kuishi kwa kukuza maisha katika sayari.

Tunahitaji Mkataba Mpya wa Kijani Ulimwenguni na mifumo ya elimu ya umma inayofundisha ikolojia ya binadamu na maadili ya uongozi ambayo yatawezesha mabadiliko haya sasa na katika siku zijazo.

 3. Haki ya kiuchumi – Kuwekeza kwenyei elimu na huduma nyingine za umma katika uchumi uliobadilishwa.

Mfumo wa uchumi lazima utosheleze mahitaji halisi ya watu wote kwa kuzingatia usawa na fursa, sio faida. Janga hili lazima liwe mwashirio wa mabadiliko ya msingi wa kutoka kwenye ubepari na kuelekea demokrasia ya mahali pa kazi na mageuzi makali ya kugawa upya uchumi unaotoa kipaumbele kwa kodi inayolenga maendeleo na matumizi ya maendeleo katika huduma za umma kwa wote, kitaifa na kimataifa. 

4. Haki ya kisiasa – Urekebishaji wa mijadalaya kisiasa katika ngazi zote 

Tunahitaji kuondokana na utawala wa kimabavu na utaifa unaojenga chuki dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa mengine. Lazima tuimarishe mshikamano wa kimataifa, kukuza ushirikiano wa kimataifa, na kuimarisha harakati za  makundi ya kimataifa mpaka kwenye mashina. Tunahitaji kutengeneza uchumi jumuishi zaidi na demokrasia shirikishi katika ngazi za mitaa, kitaifa, na kimataifa.

Mawazo haya ya awali hayaashirii ndoto za mchana au utopia; Bali yanajenga juu ya mawazo na vitendo vya makundi mengi ya wanamaendeleo na vyama duniani kote. Sisi, wahahusika tuliosaini, tunaona mawazo haya ni kwa ajili ya kufanya mtazamo mpya wa elimu na jamii kama njia muhimu ya kukabiliana na kuondokana na majanga  makubwa ambayo sayari inakabiliwa nayo.

PDF katika Kiswahili

bottom of page